Thursday , 10th Nov , 2016

Halmashauri ya Wilaya ya Mufundi mkoani Iringa imetenga milioni 150 za mapato yake ya ndani ikiwa ni asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuvipatia vikundi 89 vya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza Kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Festo Mgina.

 

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Prof. Riziki Shemdoe, amesema kuwa fedha hizo zitatolewa kwa vikundi ambavyo tayari vimeanza kufanya kazi ikiwa ni kuviendeleza pale vilipo.

Aidha Mkurugenzi Shemdoe ameongeza kuwa ameongeza kuwa halmashauri yake ilifanya mchujo kwa vikundi vinavyostahili kupata fedha hizo ili kujiridhisha na miradi wanayoifanya kuepuka miradi hewa.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema fedha hizo kwa vikundi zimetolewa milioni 1 hadi milioni 3 kwa kikundi licha ya kuwapo kwa vikundi vyenye mahitaji makubwa kulingana na miradi waliyoianzisha.

Aidha ameongeza kuwa vikundi hivyo vitakavyopewa mikopo hiyo vitapaswa kurejesha fedha hizo baada ya kufanyia kazi katika miradi yao na zikirejeshwa haraka huwa zinakopeshwa kwa vikundi vingine vyenye uhitaji.