
Meneja Mkuu wa kitengo cha Utabiri wa TMA ,Samweli Mbuya,Akizyungumza na swaandishi wa Habari(Hawapo Pichani)
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), imetoa utabiri katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu unaoonyesha kuwa kutakuwa na kiwango cha baridi katika mikoa ya nyanda za juu kusini kisichozidi nyuzi joto 12 pamoja na upepo katika baadhi ya maeneo.
Akitoa ubariri huo leo jijini Dar es salaam Meneja Mkuu wa kitengo cha Utabiri wa TMA ,Samweli Mbuya, amesema katika majira hayo ya Kipupwe mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Njombe na sehemu ya Morogoro katika wilaya ya Mahenge zinatarajiwa kuwa na kiwango cha joto la wastani
Kwa upande mwingine, Mbuya amesema kutakuwa na mvua za nje ya msimu zitakazonyesha katika mikoa ya kanda ya ziwa ambazo hazitakuwa na madhara kwa wananchi huku upepo katika ukanda wa pwani wa Bahari ya Hindi nao ukitarajiwa hivyo wavuvi pamoja na wasafiri wametakiwa kujihadhari