Waziri wa nchi ofisi ya rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene,
Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi wa ni namna gani serikali itaweza kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji leo bungeni mjini Dodoma, na kusema migogoro hiyo hasa inachochewa na maendeleo kwa kuwa kila mtu sasa anahitaji maendeleo ya haraka.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa hakuna miujiza mingine ya kumaliza tatizo hilo la migogoro iwapo wadau, wakiwemo, wakulima, wafugaji na viongozi hawatatumia busara kumaliza migogoro hiyo kama walivyokuwa wakifanya wazee wa zamani.
Waziri huyo wa TAMISEMI, amekiri kuwa tatizo hilo ni kubwa sana nchini hivyo serikali kushirikiana na wadau wanatilia mkazo kuona ni jinsi gani wataweza kutatua tatizo hili ikiwemo kuwashirikisha wadau husika na viongozi wa kimila wa maeneo yenye migogoro ya ardhi.
Mhe. Simbachawene alikua anatoa ufafanuzi baada ya kuulizwa swali na mbunge wa Kondoa Mhe. Juma Nkamia kuwa ni lini serikali itaweza kutatua migogoro ya kimuingiliano kati ya wakulima na wafugaji.