
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam, na Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano kusema kuwa serikali imeanza mchakato wa kuwataka wote wanaofanya shughuli za uzalishaji huo kupata kwanza kibali cha serikali kabla ya kuendelea na shughuli zao.
Wiraza hiyo imesema kuwa mifuko hiyo imekua ni changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa,kuchafua mandhari na kuziba mifereji hivyo kusababisha mafuriko na athari nyingine za kimazingira.
Imeeleza kuwa mwelekeo wa mazingira ya nchi yetu ni mbaya, kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini, asilimia 61 ya nchi yetu inatishiwa kuwa jangwa, ambapo kila mwaka tunapoteza takribani hekari milioni moja za misitu.
Mwaka huu hakutakua na maadhimisho ya Kitaifa Siku ya Mazingira Duniani badala yake wakuu wa mikoa wameelekezwa kwamba kila mkoa ufanye maadhimisho haya kwenye maendeo ya mikoa yao wakati Kimataifa mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyikia nchini Angola