Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi,wajumbe wa halmashauri kuu za wilaya ya Tanga,Kassi Kisauji na wa Mkinga Omari Mwasingo
Uongozi wa kiwanja cha ndege unadai kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni sehemu ya uwanja huo, wakati wananchi nao wanadai eneo hilo ni mali yao.
Wanaomba Rais Dr.John Pombe Maguful kuingilia kati mgogogro huo ili haki yao iweze kupatikana kwa kuwa hata hivyo hawana mahala pengine pa kwenda.
Licha ya kusumbuka huku na kule bado suluhu haijapatikana na hapa,wanamuomba Rais Dk Magufuli kuinhilia kati mgogoro huo.
Wamesema kuwa Wameishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 30 wakitumia eneo hilo kwa ajili ya makazi na kilimo.
Hata hivyo haijulikani watakapoenda kuishi wananchi hao ikiwa wataondolewa katika eneo hilo kwa nguvu ya dola.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga Abdullah Lutavi amesema Kata zenye mgogoro na kiwanja hicho ni Mwanzange,Duga Masiwani Shamba na Maweni kichangani.