Friday , 6th Mar , 2015

MGOGORO uliokuwepo baina ya wananchi wa mtaa wa Ranadhani halmashauri ya Njombe na mkandalasi wa umeme wa Umeme vijijini (Rea), umemalizika ambapo wananchi walikuwa wanakataa kupitishwa umeme katika viwanja vyao na sehemu wanazotaka kujenga.

Mradi wa Umeme Vijijini (REA)-Tanesco Njombe waanza kusambaza nguzo Vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Ramadhani ulikokuwa mgogoro baada ya kuonyesha eneo la kupitisha umeme unaoenda vijijini, Meneja wa Tanesco mkoa wa Njombe, Eng Andrew Kichiwa, amesema kuwa wananchi walicho kuwa wakipingana na Rea ni kupitishwa nguzo hizo katika makazi yao ambapo msanifu mradi hakuzungumza na wananchi wakati wa kuweka mradi huo.

Amesema mgogoro huo umeisha baada ya wananchi kuonyesha maeneo ambayo mradi huo unatakiwa kupita tofauti na ambapo ulitakiwa kupita awali maeneo ambayo ni makazi yao na kuonyesha maeneo ambayo ni barabara za mitaa na kupitisha umeme huo.

Kilicho leta mgogoro baina na wananchi kinadaiwa ni ushirikishwaji wa wananchi wakati wa kuweka mradi huo ambapo wananchi hawakutaka nguzo za umeme huo kusimikwa katika maeneo ambayo tayali wanaplani za kujenga.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Ramadhani, Bathomeo Kyando alisema kuwa mgogoro huo umetokana na kuto washirikisha wananchi wakati wa uwekaji wa nguzo zizo na kuwa mgogoro huo hautajitokeza tena kwa kuwa wananchi wenyewe wameonyesha eneo la kupita mradi huo.

Nao wananchi wamesema kuwa walishangaa kuona nguzo zinawekwa katika maeneo yao ambayo wanatarajia kujenga baada ya kufukuzwa na wakala wa barabara Tanzania (Tanroad) baada ya kulipwa fidia.

Wamesema kuwa kwa maeneo ambayo wameonyesha umeme upiti hawana pingamizi na umeme utapita bira ya kuwapo kwa matatizo yoyote na wao wanafurahi kuona wenzao wanapata umeme lakini kwa kupitisha katika makazi yao hawakufurahia.

Awali kulitokea nvutano baina ya meneja wa Tanesco na wananchi kuhusiana na umbali iliokuwa unatakiwa kuwapo baina ya nguzo na nyumba za watu.