Thursday , 9th Oct , 2014

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Tanzania kimepungua kutoka asilimia 6.7 mwezi Agosti mwaka huu hadi asilimia 6.6 mwezi Septemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka ofisi ya taifa ya takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka ofisi ya taifa ya takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo, ametoa takwimu hizo jijini Dar es Salaam jana kwamba mfumuko wa bei nchini ni sawa na ule wa nchi jirani ya Kenya.

Bw. Kwesigabo ameongeza kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania katika manunuzi nayo imeendelea kuporomoka ambapo hivi sasa kila shilingi mia moja inaweza kufanya manunuzi yenye thamani ya shilingi 66.7 pekee.

Kwa upande Mwingine Maduka makubwa maarufu kama supermarket yametajwa kuwa moja ya masoko muhimu kwa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali nchini Tanzania lakini viwango duni vya vifunganishio na ukosefu wa uhalisia imesababisha maduka hayo kujaa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Mkurugenzi wa jumuiya ya vikundi vya biashara ndogo ndogo Bw. Gaston Kikuwi, amesema hayo leo na kufafanua kuwa uduni wa bidhaa na vifungashio ni suala linalohitaji maboresho ya haraka ili fursa zilizopo kwenye maduka hayo ziweze kuwanufaisha wajasiriamali wa Kitanzania.