Mafuvu ya watu waliouwa wakati wa vita vya mauaji ya Kimbari
Octavien Ngenzi mwenye umri wa miaka 58 na Tito Barahira mwenye umri wa miaka 64 watajibu mashitaka ya kuwaua mamia ya wakimbizi wa Kitutsi katika kanisa la mji wa mashariki wa Kabarondo Aprili 13, 1994.
Hii ikiwa ni kesi ya pili kufanyika Jijini Paris, katika mahakama maalumu iliyofunguliwa kuwashitaki Wanyaruwanda wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo ya kimbari waliokimbilia nchini Ufaransa, inategemwa kuweka wazi mahusiano yenye mashaka baina ya nchi hizo mbili.
Rwanda bado inaendelea kuituhumu Ufaransa kushiriki katika mauaji hayo kwa kuipatia msaada serikali ya wakati huo ya Kihutu.