Saturday , 27th Dec , 2014

Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji  Israel Natse  amewataka wananchi wa jimbo hilo kuacha kuzingatia kauli yake ya kuwataka kuacha kuchangia  ujenzi wa maabara

Natse  amewataka wananchi wa jimbo hilo kuacha kuzingatia kauli yake ya kuwataka kuacha kuchangia  ujenzi wa maabara kwa shule za kata katika maeneo yao na kuwachapa viboko watendaji wa kata watakaowadai michango na badala yake kutekeleza agizo la Rais  la ujenzi huo kwani litakuwa na manufaa kwao kwa baadaye.

Hamasa hiyo ameitoa wakati alipokuwa akikamilisha kusambaza mabati 1,160 na mifuko ya saruji 950 kwa shule za sekondari za kata 21 uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 49.5 kupitia fedha za mfuko wa jimbo ili kutekeleza agizo hilo la ujenzi wa maabara hizo, ambazo baadhi yake ujenzi huo umesimama na huenda ukashindwa kukamilika kwa muda huo uliotolewa  hasa kutokana na baadhi ya wazazi kukabiliwa na michango ya karo za wanafunzi.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wakiwemo wenyeviti wa kamati za ujenzi wa maabara katika shule hizo wamesema baadhi ya shule ujenzi wake umesimama kutokana na vijiji kukosa viongozi wahamasishaji na kutawala kwa siasa.

Kwa upande wake afisa elimu shule za sekondari wilayani Karatu Bernard Mnyenyelwa akizungumzia hali ya elimu na ujenzi wa maabara hizo amesema umekamilika kwa wastani wa asilimia 62 huku shule 63 na vyumba 12 vikiwa vimekamilika lakini bado shule hizo zinategemea walimu wasioajiriwa…