Monday , 11th Mar , 2019

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini John Heche ametoa siku 14 akiitaka serikali ya mkoa wa Mara kutoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo ya Jimbo lake.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Jimboni kwake mapema jana Mbunge, John Heche amesema anatoa wiki 2 ili kuhakikisha fedha hizo za wananchi znatoka ili zifanye maendeleo ya wananchi.

Heche amesema, "Mkuu wa Mkoa wa Mara alizuia sisi kutumia pesa zetu, na akasema sisi fedha zimeibiwa kama mtu ameiba basi akamatwe lakini si kuzuia mpaka sasa hata uchafu unashindwa kuondolewa."

"Natoa wiki 2 tunataka hela zetu zitolewe tuendelee na maendeleo yeyote mje mtuhumu na wakati wa uchaguzi kwa sababu uchaguzi ni lazima" ameongeza Heche

Wakati huohuo Mbunge Heche amekabidhi mabati 100 kwa ajili ya kukamilisha vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Sirari.