Wednesday , 8th Feb , 2017

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo ameingia awamu ya pili ya kupambana na dawa za kulevya na ametaja watu wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya kwa namna moja ama nyingine.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Mchungaji Josephat Gwajima ni miongoni wa watu waliotajwa katika tuhuma hizo na kuwataka kuripoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam siku ya Ijumaa wiki hii kwa ajili ya mahojiano.

Wengine aliowataja ni pamoja na Mmiliki wa hotel ya Slip Way, Mmiliki wa MMI Wine anayefahamika kwa jina la Salehe, wamiliki wa Yatch Club, Mwinyi Machapta.

Wengine ni Mzee Kiboko anayeishi Mbezi,  Rose ambaye yuko China lakini inadaiwa kuwa ameweka makazi yake nchini Ghana, Hafidh anayeishi Mbezi Mwisho, pamoja na mbunge mstaafu Idd Azzan.

Makonda ambaye amesema siku ya leo alikuwa na orodha ya watu 65, ametajwa wengine kuwa ni Yusuph Manji, Mmiliki wa Sea Clif Hotel, Nassoro Selem wa Mabibo, Hussein Pamba Kali na mtu anayefahamika kama Bossi Kizenga wa Bunju.

Makonda ametaja pia makampuni yanayojihusisha na usafirishaji wa meli ambayo ni pamoja na ni pamoja na Tanga Petrolium Ltd, GBP Tanzania Limited

Amesema katika awamu hii, itafanyika oparesheni ya kupita nyumba kwa nyumba kuwasaka watu wote wanahisiwa kuhusika, huku akiwashuku wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kazi wanayoifanya ya kukusanya taarifa kutoka mitaani kwao.

"Awamu ya pili ya kupambana na madawa ya kulevya tumeianza leo ...Kila tunayemuita ajue tunamfahamu kuliko anavyofikiri. .....Kwenye zile nyumba ambazo wananchi mnazitilia shaka, toeni taarifa" Amesema Makonda 

Msikilize hapa RC Makonda

Paul Makonda