Mpatanishi wa Mgogoro wa Burundi Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamini Mkapa akiingia katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha
Mazungumzo hayo ya awamu ya pili yalitarajiwa kufunguliwa rasmi jana ,ambapo hadi jioni mazungumzo hayo hayajaendelea licha ya kuwapo kwa misuguano,huku kila upande ukieleza matakwa yake na baaadae baadhi ya viongozi kutoka Burundi walionekana wakitoka nje eneo la mazungumzo hayo.
Jean Diean ni kiongozi wa chama RADEDU ameeleza sababu za kusuasu kwa kuanza mazungumzo hayo, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa watu wanaohusishwa na kutaka kupindua nchi na kuongoza maandamano.
Nae Gabrel Phil ambae ni mwakilishi wa asasi za kiraia nchini Burundi akatumia nafasi hiyo kwa kuwataka wanasiasi kuachana na Itikadi za kivyama na siasa na badala yake watafute amani ya kudumu kwa manufaa ya warundi wote.
Mazungumzo hayo yalianza rasmi mapema mwezi wa tano mwaka huu na katika mazungumzo yaliotarajiwa kuendelea hii leo tayari wamewasili maraisi wa tatu wan chi ya Burundi akiwemo,DOMITIEN NDAIZEYE,MEJA PIERRE BUYOYA na SYLVRSTER NTIBATUNGAYA.

