Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Jumanne Maghembe kuwa Waziri wa Maliasilina Utalii Desemba 28,2015 Ikulu
Akizungumza mara Baada ya kuapisha jana Ikulu Jijini Dar es Salaam Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa amejipanga kuhakikisha zoezi waliloanza la kukusanya kodi linatekelezeka kwa kiwango kikubwa huku Waziri wa Elimu Dkt. Joyce ndalichako akiahidi Elimu bora kwa Watanzania.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Pro. Jumanne Maghembe amewataka watanzania wamuamini katika wizara hiyo kwa kuwa ndio ana utaalamu nayo huku akiwatangazia kiama wanaofanya Ujangali.
Mawaziri walioapishwa ni Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Elimu ya Ufundi Mh. Joyce Ndalichako, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Gerson Lwenge na Waziri wa Mali Asili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Hamad Juma Masauni.