Tuesday , 31st May , 2016

Leo ikiwa ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya Tumbaku Duniani, Mkurugenzi wa Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku nchini Tanzania, Dk. Lutgard Kagaruki amesema kuwa matumizi ya Tumbaku nchini bado ni janga la kitaifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku nchini ,Dk. Lutgard Kokulinda Kagaruki.

Akizungumza na East Africa Radio, leo Mkurugenzi huyo amesema kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania imeonekana kusuasua kudhibiti matumizi na Kilimo cha bidhaa hiyo hali inyopelekea watu wengi zaidi kuathirika na matumizi ya bidhaa hiyo.

Bi. Kagaruki amesema kuwa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani limetangaza matumizi ya Tumbaku ni janga la Kimataifa ambapo zao hilo lina athiri karibu kila nyanja ya jamii ikiwemo Afya, Mazingira, na Biashara kwa Ujumla.

Amesema kuwa wanaharakati wa Tanzania wanakutana na changamoto kubwa katika kupambana na matumizi ya bidhaa hiyo kutokana na Tanzania kukosa sheria madhubiti ambayo inaelenga kupambana na matumizi ya Tumbaku nchini.

Aidha, Mwanaharakati huyo ameongeza kuwa anasikitishwa na serikali ya Tanzania jinsi ambavyo inasisitiza kilimo cha Tumbaku nchini wakati nchi nyingine za Afrika Mashariki zikijairibu kudhoofisha kwa kiasi kikubwa kilimo na matumizi ya bidhaa zitokanazo na Tumbaku.

Amesema Kauli Mbiu ya Mwaka huu katika maadhimisho ya Siku ya Kupinga Matumizi ya Tumbaku ambapo yanaadhimishwa wakati Tanzania ikiwa nyumba sana kuliko nchini nyingine yoyote ni “Jitayarishe kwa pakiti zisizo na Matangazo wala Vichocheo Vyovyote.(Get Ready for Plain Packaging).