
Wakizungumza katika mkutano wa mwaka wa Vijana wa umoja wa mataifa unaofanyika jijini Arusha viongozi wa vikundi vya vijana na wadau wanaosaidia kundi hilo wamesema, jitihada za ziada zinahitajika kushughulikia changamoto za vijana ili kuwaepusha kutumiwa vibaya na makundi mengine .
Wadau hao Bw. Ismail Ramadhani kutoka Taasisi ya vijana Tanzania na Sarafina Mkuwa kutoka Amref wamesema inasikitisha kuona makundi ya watu yenye uwezo wa kulisaidia kundi la vijana kujinasua na umaskini, yanawageuza vijana kuwa kinga ya maslahi yao bila kujali madhara wanayoyapata.