Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga
Waziri Kitwanga ameyasema hayo leo wakati akitoa ufafanuzi wa namna wizara hiyo ilivyoboresha usalama wa nchi hasa maeneo ya mipakani ambapo ndio maeneo ambayo wahamiaji wengi haramu wanapita kuingia nchini.
Aidha Waziri huyo wa Mambo ya ndani amesema kwakuzingatia usalama wa Raia ofisi yake imeagiza askari nchini kufanya uchunguzi zaidi kwa kila mkoa kufichua na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika na kujihusisha na vitendo vya kuwahifadhi wahamiaji haramu nchini na kuwasafirisha
Tanzania kwa sasa ina jumla ya wakimbizi takribani laki 2 na elfu 18 na mia sita kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).