Wednesday , 15th Jun , 2016

Kufuatia kuwepo na kundi kubwa la vijana wanaokamata madereva Bodaboda na Bajaji wanaoingia maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam, Kampuni iliyopewa mamlaka ya kukamata madereva hao ya Tambaza Auction Mart and General Broker imejitokeza.

Kufuatia kuwepo na kundi kubwa la vijana wanaokamata madereva Bodaboda na Bajaji wanaoingia maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam, Kampuni iliyopewa mamlaka ya kukamata madereva hao ya Tambaza Auction Mart and General Broker imejitokeza mbele ya vyombo vya habari kusema ilishasitisha zoezi hilo tangu 27 April mwaka huu.

Afisa habari wa kampuni hiyo Bw Issa Ramadhani amesema kuwa walifikia hatua ya kusitisha huduma hizo kwa sababau za kiusalama na waliandika barua kwa Mkurugenzi wa jiji kusitisha huduma hizo na kupeleka nakala kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Kamanda wa polisi kanda maalum, Mkuu wa wilaya Ilala,Rpc Ilala, OCD Central,OCD Msimbazi,OCS Central polisi na OCS Msimbazi.

Aidha amesema kuwa watu wanaoendelea kukamata pikipiki na bajaji zinazoingia maeneo ya katikati ya mji kwa kipindi hiki si wafanyakazi wa kampuni hiyo labda ni matapeli hivyo wananchi wanatakiwa wawaepuke.