Hayo yamesemwa na Meneja Tafiti na Fedha toka Soko la hisa la Dar es salaam Ibrahim Mshindo wakati wa Uzinduzi wa Shindano la kampuni bora100 ya kati zinazofanya vizuri kwa kutoa ajira, kutengeneza faida na zinazokaguliwa mahesabu yake kila mwaka.
Mshindo ameongeza kuwa kuna kampuni 7 tu za Serikali zinazofanya vizuri sokoni na kulipa kodi kubwa hivyö ni wakati sasa kwa Serikali kuyapeleka na makampuni mengine katika soko la DSE ili yakuze mitaji yaö na kuöngeza ushindani.
kukuza mapato yao na hivyo kutengeneza faida na kuongeza ajira zaidi kwa watanzania, waandaaji wa shindano hilo wamewataka wamiliki wa makampuni ya kati yenye mauzo kati ya Bilion 1 kwa mwaka kujitokeza kwa wingi.