Wednesday , 30th Dec , 2015

Baadhi ya mashine zilizonunuliwa kwa mkopo kwa ajili ya kiwanda cha Urafiki Jijini Dar es Salaam hazijafungwa kwa muda ili kuanza kutumika kusaidia kiwanda hicho kuboresha uzalishaji.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwajage

Hali hiyo imebainika katika ziara ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage aliyoifanya katika kiwanda hicho ambacho kimedorora katika uzalishaji.

Mbali na hilo baadhi ya mashine zimeibiwa na nyingine vipuli vyake kuuzwa kama chuma chakavu na hali iliyochangia kushusha ufanisi wa kiwanda cha Urafiki.

Kusuasua kwa uzalishaji wa kiwanda hicho kumepelekea wafanyakazi kupunguzwa kazi kutoka idadi ya 3,000 hadi kubakia 800 pekee.