Monday , 2nd Jul , 2018

Baadaya kuibuka kwa mjadala kupitia mitandao ya kijamii juu ya picha ya nyumba iliyoandikwa paua kwa paa la kahawia, ambayo ilielezwa kuwa ni moja kati ya nyumba inayojengwa jijini Dodoma.

Masharti ya Ujenzi katika Jiji la Dodoma (kulia), na nyumba iliyoandikwa paua kwa paa la kahawia, ambayo imezua mjadala katika mitandao ya kijamii

Www.eatv.tv imemtafuta Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi, ambaye ameelezwa kuwa, ni kweli na kwa hadhi ya Jiji la Dodoma inatakiwa kuwa tofauti kwa kila kitu hasa muonekano kwakuwa ndio makao makuu ya Nchi, na inatakiwa ipambe kwa rangi na muonekano wa majengo yaliyo katika mpangilio unaovutia.

Kunambi amesema kuwa, suala hilo sio jipya kwakuwa sheria namba nane ya mipango miji ya mwaka 2007, imeeleza mamlaka ya upangaji miji inaweza kupangilia hadi urefu wa majengo.

“Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilikubaliana kupitia kikao cha baraza la madiwani, kuwa wata toa elimu kwa wananchi kuhusiana na mabadiliko hayo lakini pia kupaka rangi mabati kwa mitaa tofauti”, amesema Kunambi.

Kunambi ameongeza kuwa mfumo huo mpya umekuwa na changamoto, kwakuwa watu wameona kama ni kitu kipya lakini ni kutokupitia tu sheria za mipango miji, hakuna kitu kipya.