Wednesday , 24th Jun , 2015

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, amepiga marufuku vyama vya siasa vinavyotafuta umaarufu kwa kuitisha maandamano yasiyo na tija na kusema atakayethubutu atakutana na mkono wa dola.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas.

Sabas amesema ni vizuri viongozi wa siasa wakatumia muda mchache wa uongozi waliobakiza, kuhamasisha biashara na shughuli za maendeleo, kuliko kujikita katika vurugu za maandamano ambayo mwisho wake utakuwa mbaya kwao.

Kuhusu tuhuma za kupokea rushwa polisi katika uandikishwaji wapiga kura, amesema ni uongo na wamezoea CHADEMA kuwazushia mambo ya uongo kila wakati na sasa wanaona ni kawaida kama watani wa jadi wanavyoishi.

Amewatia moyo wananchi wajiandikishe na askari wapo kuwalinda na kuhakikisha amani inakuwepo na atakayejitokeza kuvuruga zoezi hilo atakumbana na mkono wa dola.

Akizungumzia juu ya lengo la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kufanya maandamano kupinga masuala yanayoendelea katika vituo vya uandikishwaji vinavyofanywa na polisi na amesisitiza lengo liko palepale na amewataka polisi kujiandaa ipasavyo.

Amesema kwa sasa wanachofanya kukusanya taarifa za wangapi wamebaki katika maeneo ya kujiandikisha na walioandikishwa,ili wanapoandamana wanapata hoja za kuzungumza kwa wananchi.