Thursday , 24th Nov , 2016

Marubani wa shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa wako katika mgomo na kusababisha kukwama kwa mamia ya wasafari na safari za ndege kusitishwa baada ya chama cha marubani kuitisha mgomo utakaokoma hapo kesho.

Marubani nje ya ofisi za shirika hilo katika mgomo wao

Shirika hilo kubwa la ndege duniani lililazimika kusotesha safari za ndege 900 hapo jana na safari nyingine 912 hii leo na kusababisha abiria 200,000 kukwama.

Mgomo huo ni wa 14 tangu mwezi April mwaka huu.

Msemaji wa umoja wa marubani Joerg Handwerg amesema uongozi wa shirika hilo haujaonesha dalili za kuwa tayari ya kutoa ofa ambayo itakuwa msingi wa majailiano.

Mamia ya abiria wakiwa wamekwama uwanja wa ndege kutokana na mgomo huo