Askari wa Kikosi cha Mbwa akiwa katika Mazoezi ya Mbwa(picha kutoka Maktaba)
Akipokea msaada huo Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amesema kuwa tatizo la biashara haramu litakuwa historia kwa kuwa licha ya msaada wa mbwa hao pia serikali kupitia wadau wengine wa maendeleo imejipanga katika kukabiliana na uhalifu huo.
Aidha Prof Maghembe ametumia fursa hiyo kuwashukuru wamarekani kwa msaada huo waliotoa lakini pia katika kudhibiti ujangili nchini amesema wamekwishaanza kurusha ndege zisizo na rubani katika kupiga picha katika mbuga za wanyama katika operesheni maalumu ya kukomesha Ujangili.
Naye Naibu IGP nchini Abdulrahman Kaniki ameishukuru serikali ya Marekani kwa msaada huo na mafunzo ya uendeshaji wa mbwa kwa maafisa wa nne waliyoyapata nchini Marekani huku akiahidi kuwa jeshi la polisi litawatunza mbwa hao kwa uangalifu mkubwa.
Mbwa hao watatumika kwa ajili ya ulinzi katika maeneo ya bandari ya Dar es salaam, na viwanja vya ndege nchini huku serikali ya Marekani ikiahidi kwamba hapo baadaye watatoa mbwa wengine na mafunzo kwa maafisa polisi kwa ajili ya bandari za Tanga na Mtwara ambazo nazo ni chanzi kikubwa cha mapato nchini.