Friday , 16th May , 2014

Mke wa hayati mwalimu Julias Nyerere, mama Maria Nyerere amewaasa vijana nchini kutojiingiza katika malumbano yasiyokuwa na tija kiasi cha kuwatukana waasisi wa taifa ili kuliepusha taifa kuingia katika hali ya uvunjifu wa Amani.

Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere

Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ameitaka Serikali ya Tanzania kuchukua tahadhari kutokana na kuwepo kwa hatari ya kuibuka vita nchini sambamba na taifa kuingia katika wakati mgumu hali inayosababishwa na mitafaruku mbalimbali pamoja na baadhi ya viongozi kukosa busara na taifa kutomtii Mungu.

Mama Maria Nyerere ameyasema hayo na mengine mengi leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na vijana mbalimbali waliofika nyumbani kwake Msasani kuongea naye na kupata ushauri kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini

Hata hivyo Mama Maria amesema kuwa hashangazwi na yale yanayotokea nchini kwa sasa ambapo viongozi na waasisi wanatukanwa kwani hilo linatokea sehemu mbalimbali nchini hivyo anaendelea kusisitiza watanzania walirudishe taifa mikononi mwa Mungu.