
Chini ya mpango huo Serikali ya Syria utasitisha mapigano katika maeneo mahususi yanayoshikiliwa na wapinzania ambapo Marekani na Urussi zitaanzisha kituo kitakachoratibu mapambano dhidi ya kundi la Dola ya Kiislamu IS na wapiganaji wa al-Nusra..
Tangazo hilo la kusitisha mapigano linafuatia mazungumzo kati ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry na waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Urussi Sergei Lavrov.
Mpango huo utawalazimu makundi yote yaan Seriali na upinzani kukutana na kuanisha matakwa yao.