
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akikabidhi mabasi kwa Jeshi Mkuu huyo wa mkoa amesema zoezi hilo litakuwa endelevu baada ya kuanza rasmi jumatatu na kuzitaka taasisi za kidini nchini kuongoza ibada kwa waumini wao ili kuepuka vitendo hivyo kwa kile alichokieleza kuwa ni vitendo vya laana.
“Niwaombe, leo ijumaa na watakaosali jumamosi na jumapili waongoze ibada ya kutubu kama mkoa na kuomba rehema ya mungu tuishinde hii vita, ndugu zangu niwaambie hili jambo limelaaniwa tangu kwenye biblia” amesema Makonda
“Juzi nilivyotoa maelekezo vyombo vikubwa vya habari viliniweka mjadala, Na kuna mtu alinambia mbona naweka maisha yangu yako hatarini, nikamwambia hapama ila ndiyo nakuwa salama zaidi mbele ya mungu." Amesema Makonda
Oktoba 31 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Paul Makonda alisema "leo zimefika ujumbe 18972 na hawa wote wanalaani na simu zilizokuwa zinapigwa ni nyingi sana niwasihi endeleeni kutuma ujumbe ili tuendelee kukomesha biashara hiyo haramu".
"Lakini kwenye hiyo orodha kuna majina yako 200 lakini kuna baadhi ya watu wamejirudia kwa sababu wameamua kujitangaza watu hao ni James Delicious, Dida Mtamu, Aunty Miliki, Abbasi”.Aliongeza Makonda