
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Kupita ukurasa wake wa instargam anaoutumia kwa jina la 'Baba Keagan', Makonda ameeleza kutofurahishwa na mwenendo wa uendeshaji wa mradi huo ambao ulitabiriwa kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa maeneo wa Kimara wanoelekea katikati ya mji.
"Sifurahishwi namna mradi wa mwendokasi unavyoendeshwa kwani matarajio ya Mh. Rais ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri Kwa wananchi wa Dar es Salaam ikigeuzwa historia kupitia mradi huu ", ameandika.
"Kwasababu hizo nimeagiza watendaji wote wanaosimamia mwendokasi niwakute Kimara stand ya mwendokasi kesho Saa 12:30 asubuhi wanieleze kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukua huku wakishuhudia kero wanazopitia wananchi", ameongeza katika taarifa hiyo.
"Nitumie pia fursa hii kuwaomba radhi wananchi Kwa kero hii na niwaahidi kuwa jambo hili litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni. Tukutane mapema asubuhi mwendokasi Kimara".