Friday , 2nd May , 2014

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewakumbusha Watanzania kuwa wazalendo na nchi yao ikiwa ni pamoja na kukataa matendo ya kutoa ama kupokea rushwa ili kudumisha haki na usawa katika Taifa.

Makamu wa rais wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal.

Akizungumza mapema leo katika maadhimisho ya uzinduzi wa mbio za Mwenge kitaifa yaliyofanyika mkoani Kagera, Dkt. Bilal amesisitiza umuhimu wa uzalendo na kudumisha Muungano

Dkt. Bilal amesema Watanzania wanatakiwa kuwa watulivu hasa wakati huu ambapo Katiba mpya ya nchi inaendelea kutungwa .