Aliyejitokeza wa kwanza hii leo ni ni mtumishi wa CCM Idara ya Siasa na Uhusiano wa Tanzania, Amos Siyantemi ambaye ameahidi kudumisha amani na utulivu uliopo nchini huku akitumia kauli mbiu yake ya Sura mpya, Fikra mpya.
Siyantemi alifuatiwa na makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ambaye akiongea na waandishi wa habari amesema atahakikisha anaulinda muungano uliopo nchini kwa kuwa ni wa kipekee ulimwenguni pamoja na kudumisha umoja, ulinzi na mshikamano.
Kada mwingine wa CCM aliyechukua fomu za kuwania urais hii leo ni Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambaye amesema atahakikisha watumishi wa umma hawajihusishi moja kwa moja na biashara na atakayefanya hivyo atakuwa amekosa sifa ya kuwa mtumishi wa umma. Mgombea mwingine aliyechukua fomu za kuwania urais ni Balozi Ally Karume.
John Pombe Magufuli pia amechukua fomu na kusisitiza kuwa yeye hana kipaumbele zaidi ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi. amesema "Kipaumbele changu ni Ilani ya CCM" na mwingine ni waziri mkuu aliyejiuzulu Mh. Edward Lowassa.