Thursday , 15th Oct , 2015

Mahujaji wengine wawili kutoka Tanzania ambao walikuwa hawajaoneka toka ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makka nchini Saudia Arabia wametambuliwa kuwa ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (katikati) akielezea jambo

Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia 22 baada ya wengine 20 walishatambuliwa katika zoezi la Kwanza la uokozi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa imetaja majina kamili ya mahujaji hao ni Hafsa Sharif Salehe Abdallah na Khadija Hamad Hemed.

Ajali hiyo ya Kukanyagana Mahujaji ilitokea tarehe 24 Septemba mwaka huu na kupelekea zaidi ya watu 400 kufariki dunia kutoka mataifa mbalimbali duniani wengi wao wakitokea katika taifa la Iran.