Friday , 10th Jun , 2016

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imetoa agizo kwa wanafunzi wanne waliofukuzwa Chuo Kikuu cha St. Joseph kuwawakilisha wenzao 316 katika kesi ya kuishtaki tume ya Vyuo Vikuu TCU na chuo hicho, kwa kuwapa masomo hewa.

Wakili anayewatetea wanafunzi hao, Wakili Msomi Emanuel Augustino Muga amewaambia waandishi wa habari kuwa, Jaji Elieza Felesh amekubali ombi la wanafunzi hao na hatua inayofuata nikuanza kusikilizwa kwa kesi ya msingi ya fidia kwa wanafunzi hao.

Naye jaji anaye sikiliza kesi hiyo jaji Elieza Felesh amezitaka pande zote mbili kuto chukulia shauri hilo kwa mlengo wa kisiasa na kuiachia mahakama kuamua hatua za kisheria kuchukua mkondo wake.