Tuesday , 24th Nov , 2015

Mahakama kuu kanda ya Mwanza leo inatarajiwa kutoa maamuzi ya kuagwa ama kutoagwa kwa mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wakili wa upande wa mlalamikaji John Malya akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuairishwa kwa kesi hiyo hapo jana.

Mahakama kuu kanda ya Mwanza leo inatarajiwa kutoa maamuzi ya kuagwa ama kutoagwa kwa mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Alphonce Mawazo aliyeuawa na watu wasiojulikana Novemba 14, mwaka huu.

Ombi la shauri la kupinga amri ya polisi kuzuia kuagwa kwa mwenyekiti huyo jijini Mwanza ilifikishwa na baba mdogo wa Mawazo Mchungaji Charles Lugiko, dhidi ya walalamikiwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza na mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Baada ya Ombi hilo kukubaliwa mbele ya jaji Lameck Mlacha wa mahakama hiyo leo inatarajiwa kutolewa kwa maamuzi kama mwili huo utaagwa Mwanza au la.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Jaji Mlacha kukubali kusikiliza shauri hilo la madai, mmoja wa mawakili wa upande wa mlalamikaji John Malya alisema kuwa ombi limefikishwa kwa ofisi ya mwanasheria mkuu na kuwa leo utatolewa uamuzi.