Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na Mama Janeth Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema hayo wakati wa ibada ya kumbumbuku ya miaka 32 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini.
Rais Magufuli amesema kuwa anamkumbuka kiongozi huyo wa Zamani wa Tanzania kama kiongozi shupavu aliewapenda watanzania na aliechukiwa rushwa na kuwatumikia watanzania kwa moyo wote.
Kwa upande wake rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa amesema kuwa mfumo ulitumika kumpata kiongozi wa nchi wa sasa ndio mfumo uliotumika kumpata Waziri huyo Mkuu wa Zamani.
Aidha Mhe. Mkapa amesema kuwa Watanzania wamuache rais Magufuli arudishe heshima kwa taifa katika utumishi wa umma ambao wengi wao walikuwa wamejisahau katika utendaji wao.
na Askofu Mkuu wa jimbo la Katoliki la Dar es Salaam, Muadhama Policarp Kadinali Pengo ameeleza mchango wa Sokoine katika maendeleo ya Taifa na kusema mfano wake ndio aliokuwa nao rais wa sasa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.






