Saturday , 24th Feb , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amerejea nchini kutoka nchini Uganda alikokuwa kwenye kutano wa wkuu wa nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano huo ambao ulihusisha viongozi wa mchi zote za Jumuiya ya Afrika Mshariki, ulikuwa ni wa siku 2, ambapo pia alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Aliporejea akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza amepokelewa na mkuu wa mkoa huo John Mongela, na kujadili schangamoto mbali mbali zinazoukabili uwanja huo ikiwemo ujenzi wa jengo la abiria, ambalo ameahidi kulifanyia kazi.

Soma hapa taarifa yote