Friday , 11th Nov , 2016

Rais wa tanzania Dkt. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir.

Marehemu Hafidh Ali Tahir

Kifo hicho kilitokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.

"Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.

Rais John Magufuli

"Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.