Thursday , 25th Feb , 2016

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki rais Dkt. John Magufuli amehakikishiwa kuwa maandalizi ya mkutano wa jumuiya hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi Jijini Arusha yamekamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Akizungumza mara baaada ya kukutana na Rais Magufuli Jana Ikulu Jijini Dar es salaam Katibu mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera amesema kuwa wamezungumzia uendelezaji wa viwanda ndani ya jumuiya hiyo.

Aidha Dkt. Sezibera ameongeza kuwa pia wameshakamilisha mikataba ambayo wataizungumzia katika mkutano huo ikiwemo ya umoja wa forodha pamoja na kuwa na sarafu ya pamoja na uboreshaji wa reli ya kati.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kiamtaifa Dkt. Augustine Mahiga ameeleza mambo mbalimbali yatakayofanyika wakati wa mkutano huo ikiwemo kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali.