Wednesday , 24th May , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -  anayeshughulikia Elimu.

Rais Magufuli

Kabla ya uteuzi huo Bw. Tixon Tuliangine Nzunda alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -  akishughulikia Elimu Bw. Bernard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi huu unaanza mara moja.