Thursday , 28th Jan , 2016

Halmashauri ya Wilaya ya Magu ina upungufu wa zaidi ya nyumba za walimu 1183 kati ya nyumba 1487 ambapo mpaka sasa nyumba za walimu zilizopo katika halmshauri hiyo ni nyumba 284 tu hali inayowafanya walimu wengi kufundisha katika mazingira magumu.

Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo.

Akiongea namna Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba za walimu na kuwaboresha mishahara walimu Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo amesema serikali inaendelea kuongeza bajeti katika halamshauri mbalimbali ili kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu.

Mhe Jaffo amesema kuwa kwa Serikali imekua ikiendelea kuboresha mishahara katika sekta mbalimbali hususani sekta ya walimu kutokana na watumishi wengi wa umma kufanya kazi katika mazingira magumu.

Aidha Mhe Jaffo ameziagiza halmasharu za Wilaya nchini kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa mfumo wa kieletroniki ili kuweza kukamilisha miradi mbalimbali ya kimaenndeleo katika halmashauri zao.