Thursday , 28th Jul , 2016

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, amewataka wasimamizi wa uvunaji wa misitu kuhakikisha kuwa mapato yote ya serikali yatakayopatikana yanakusanywa kikamilifu na kulipwa kama ilivyopangwa.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe.

Prof. Maghembe amesema hayo Jijini Tanga wakati wa Mnada wa Shamba la Miti la Longuza lilipo wilayani Muheza Mkoani Tanga ambalo shamba hilo ni maalumu kwa ajili ya uvunaji wa miti.

Aidha Waziri Maghembe amewataka wanunuzi wa bidhaa hiyo ya magogo ni pamoja na kuyasafirisha kwa uwazi lakini pia kuhakikisha kila mtu anahusika na uvunaji wa magogo hayo anapata kibali cha magogo yote anayo yasafirisha.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu, ambapo lipo Shamba hilo amesema kuwa anatumai shamba hilo litakuwa Mkombozi wa wana Muhuza katika kupunguza ajira kwa kupewa kipaumbele cha kuajiriwa kwa zile kazi zinazoweza kufanywa na wananchi wa kawaida.

Sauti ya Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe