Monday , 17th Dec , 2018

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike amewaagiza wakuu wa magereza kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais John Magufuli la ujenzi wa nyumba za askari wa jeshi hilo nchini kote kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani.

Rais, Dkt. John Magufuli.

Akizungumza jijini Dodoma  baada ya kukagua kiwanda cha ufyatuaji wa matofali na ujenzi wa nyumba za maafisa na askari katika gereza la Isanga, Kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi nyumba za askari ni kipaumbele cha kwanza kufuatia agizo la rais wakati anamuaapisha.

Aidha Kamishna Kasike "Suala la utatuaji wa changamoto za uhaba wa nyumba za askari litiliwe mkazo na kupewa kipaumbele ambapo kipaumbele namba moja ni  matumizi ya wafungwa katika suala la ujenzi na uzalishaji wa chakula".

Julai 14 mwaka huu wakati akimuapisha Kamishna  Jenerali Kasike, Rais Magufuli alilitaka jeshi la magereza kufanya mabadiliko kwa kuhakikisha linatumia fursa ya wafungwa kutatua changamoto ya makazi ya maafisa na askari.