Wednesday , 6th Jul , 2016

Serikali ya Tanzania imeviagiza vyombo vya dola kuendelea kuwadhibiti madereva wasiofuta utaratibu wa sheria za barabarani.

Serikali ya Tanzania imeviagiza vyombo vya dola kuendelea kuwadhibiti madereva wasiofuta utaratibu wa sheria za barabarani na kuhatarisha maisha ya watanzania kutokana na uzembe na uvunjaji wa sheria.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akieleza masikitiko ya serikali kuhusiana na vifo vya watu 30 pamoja na majeruhi zaidi ya 50 vilivyosababishwa na ajali ya kugongana uso kwa uso kwa mabasi mawili ya City Boy mkoani Singida.

Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Tanzania Mohamed Mpinga amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani katika kusheherekea siku kuu ya Eid el Fitri na kuwataka madereva wajiepushe na kutumia vilevi, kukiuka sheria za usalama barabarani.