Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Tanzania Mohammed Mpinga.
Afisa kutoka Chama cha Kutetea Abiria CHAKUA Bw. Gervas Rutaguzinda amesema hayo katika mahojiano na East Africa Radio, wakati wa zoezi la ukaguzi wa leseni kwa madereva wa mabasi yanayotumia kituo hicho, zoezi lililoendeshwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na CHAKUA.
Hata hivyo, baadhi ya madereva wamelalamikia zoezi hilo kuwa limeleta usumbufu kwao kwani sio nyakati zote wanaweza kutembea na nyaraka kama vyeti vya vyuo vya udereva walikosemea udereva kama ambavyo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamekuwa wakihitaji kuonyeshwa.
Wakifafanua kuhusu kero zinazotokana nazoezi hilo, maderva hao wamesema sio rahisi kw amtu kutembea na nakala ya nyaraka za chuo alichosomea udereva ambapo wamesema ni rahisi kwa idara husika kuhakikisha kuwa hakuna vitendo vya kughushi au utengenezwaji wa leseni bandia.