Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Madaktari wa Tanzania wapingwa Kenya

Sunday , 19th Mar , 2017

Umoja wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya,(KMPDU), umepinga vikali hatua ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina madaktari wengi ambao hawaajiriwa.

Ouma Oluga (Kushoto)

Kupitia kwa Katibu Mkuu wa umoja huo, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kwamba, Serikali ya Kenya haijawa makini katika kushughulika na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo.

Akizungumza na mtandao wa The Star wa nchini Kenya Bw. Oluga amesema, hata hivyo, watawakaribisha madaktari kutoka Tanzania na kuwaunganisha katika umoja huo na kwamba watapaswa kupitia mitihani itakayoandaliwa na Bodi ya Wauguzi.

Amesema mitihani hiyo itachukua siyo chini ya miezi mitatu labda kama tu hitaji hilo halitaangaliwa.

Bw. Oluga amedai kwamba, Kenya ina zaidi ya madaktari 1,400 ambao wanasubiri ajira, hivo itakuwa, gharama kubwa na dalili ya kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na madaktari 500 wa Kitanzania kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku.

Mapema jana Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alikubali na kuridhia ombi la Serikali ya Kenya na kuahidi kutuma madaktari 500 kusaidia kukabiliana na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo kufuatia mgomo wa madaktari ulioisha hivi karibuni baada ya kudumu kwa siku 100.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine