
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Madaktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali za Muhimbili, Aga Khan na Kenyatta nchini Tanzania wanatarajia kuendesha zoezi la upasuaji wa viungo vilivyotokana na ajali au majanga ya moto.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo Daktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali ya Muhimbili Dkt. Edwin Mrema amesema upasuaji huo utawalenga wanawake na watoto kwa wale ambao wamepatwa na majanga hayo na kushindwa kufahamu kwamba viungo hivyo vinaweza kurekebishwa na kuwa katika hali ya kawaida.
Dkt. Edwin amesema bado ufahamu kwa wananchi waliopata majanga hayo ni mdogo hivyo kupitia kambi watakayoiweka wataweza kuwasaidia kwa kufanya upasuaji bila ya malipo na kurudishia viungo hivyo katika hali ya kawaida.