Friday , 29th Jul , 2016

Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA), Mkoani Dodoma,kimeitaka serikali kusaidia kushawishi benki zinazotoa mikopo ya uwekezaji kwenda Dodoma kutoa nguvu kuwekeza kwenye rasilimali.

Mnara wa Alama ya Dodoma.

Akizungumza Mkoani Dodoma, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TCCIA, Dodoma, Fred Azaria, amesema ujio wa makao makuu ni fursa ya biashara kwa sekta binafsi kwa itaongeza idadi ya watumishi na wakazi wa mji.

Azaria amesema kuwa taasisi za kifedha zilizopo Dodoma ziwe wazi zaidi kutangaza mikopo yao na kutoa elimu kuhusu taratibu za kupata mikopo pamoja na kulegeza masharti yake ili watu wanufaike zaidi.

Katika hatua nyingine wadau kujipanga na kuweka mzingira wezeshi ya kufanikisha uhamiaji wa serikali kwenda Dodoma ikiwemo urahisishaji wa upatikanaji ardhi kwa ajili ya wajasiriamali na mtu mmoja mmoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za biashara na makazi