Wednesday , 16th Sep , 2015

Tume ya taifa ya uchaguzi imesema maandalizi ya uchaguzi yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 50 baada ya kupokea sh bilioni 72 za ufanikishaji wa zoezi hilo kwa kusambaza vifaa vya uchaguzi mikaoni.

kurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhan.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Jana Mkurugenzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani ambapo amesema kuwa vifaa vingine vishaanza kusambazwa mikoani na zoezi la mwisho litakua ni kupeleka karatasi za kupigia kura huku utata wa majimbo akisema umekwisha tatuliwa.

Aidha Bw, Kailima pia alitolea ufafanuzi suala la jimboo la Lushoto ambalo Mgombea wake mmoja alifariki na kusema kuwa uchaguzi wa jimbo hilo utasogezwa mbele huku akitolea ufafanuzi zaidi wa kisheria juu ya mgombea yoyote anapofariki.

Kailima aliongeza kuwa kwa wale wanachuo ambao siku ya kupiga kura itawakuta tofauti na maeneo waliojiandikishia walitakiwa kuhakiki katika vituo walivyopo sasa ili waweze kupiga kura za wagombea wa nafasi zote katika eneo alililopo.