Thursday , 15th Oct , 2015

Tume imetoa maamuzi ya kisera yanayoelezea mambo ambayo yatamfanya mpiga kura aweze kuruhisiwa kupiga kura au kuzuiliwa kupiga kura kutokana na changamoto mbalimbali.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva

1.CHANGAMOTO
Kutofautiana kwa namba ya kadi ya mpiga kura ile iliyopo kwenye Daftari la Kituo wakati taarifa nyingine zote zimo kwenye Daftari.
ATHARI
Wapiga kura wenye sifa za kupiga kura kukosa haki ya kupiga kura.
MAAMUZI
Kwa Mpiga Kura ambaye atakuwa na kadi ya Mpiga Kura ila namba ya kadi ikatofautiana na namba iliyo kwenye Daftari la Kituo: Aruhusiwe kupiga kura.

2.CHANGAMOTO
Kutoonekana vizuri au kutoonekana kabisa kwa picha ya mpiga kura aliyejiandikisha katika kadi ya mpiga kura ili hali taarifa zake nyingine ziko kwenye daftari la kituo sawa na zile zilizoko.
ATHARI
Wapiga kura wenye sifa za kupiga kura kukosa haki ya kupiga kura kwa picha zao kutoonekana kwenye daftari la kituo.
MAAMUZI
Kwa wapiga kura ambao picha zao hazikuonekana vizuri au kutoonekana kabisa kwenye kadi ya mpiga kura: Waruhusiwe kupiga kura hata pale ambapo picha zao hazitatokea kwenye daftari.

3.CHANGAMOTO
Mabadiliko ya mipaka ya kiutawala yaliyofanyika wakati au baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika.
-ATHARI
Majina ya maeneo mapya ya kiutawala kutofautiana na majina yaliyopo kwenye kadi za wapiga kura.
-MAAMUZI
Kwa wapiga kura walioandikishwa na tume waliopo kwenye maeneo mapya kiutawala na majina ya maeneo hayo yanatofautiana na majina yaliyopo kwenye kadi zao: Waruhusiwe kupiga kura.

4.CHANGAMOTO
Wapiga Kura wasioonekana kwenye Mfumo wa daftari lakini wana vitambulisho vilivyotolewa na tume na fomu zao za kuandikishwa kufikishwa tume.
-ATHARI
Wapiga kura hao kukosa haki ya kupiga kura kwa kuwa majina na picha zao hazionekani katika mfumo wa Daftari.
-MAAMUZI
Majina ya wapiga kura hao kuandaliwa katika mfumo wa orodha bila kuwa na picha na kupelekwa katika vituo walivyojiandikisha: waruhusiwe kupiga kura.

5.CHANGAMOTO
Wasio na kadi za kupiga kura lakini majina yao yapo kwenye daftari.
-ATHARI
Hawataweza kupiga kura kwa kuwa hawana kadi.
-MAAMUZI
Wapiga kura ambao majina yao yamo kwenye daftari la kituo lakini hawana kadi ya kupigia kura: Wasiruhusiwe kupiga kura.

6.CHANGAMOTO
Wapiga kura wenye kadi za kupigia kura lakini taarifa zao hazipo katika daftari la kudumu la wapiga kura.
-ATHARI
Hawataweza kupiga kura kwa kuwa hawapo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
-MAAMUZI
Kwa wapiga kura ambao wana kadi ya kupigia kura lakini hawapo katika daftari, wasiruhusiwe kupiga kura.