Thursday , 1st Dec , 2016

Tanzania leo inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Abood amewataka wananchi visiwani humo kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Abood

Mhe. Abood amesema kuwa kuwepo kwa tabia hatarishi kwa vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24 inachangia ongezeko la kuenea kwa virusi vya Ukimwi visiwani Zanzibar.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Visiwani humo Waziri Abood, amesema kuwa maambukizi ya Ukimwi kwa vijana yanaongezeka kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya kujamiiana kwa jinsia moja pamoja kuongezeka kwa maeneo yaa starehe.

Wakati huo huo Abood ametoa taarifa maalumu ya siku ya watu wenye ulemavu na kusema kuwa serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kundi hilo linapata haki zake zote na fursa za sawa kama raia wengine.