Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania Mhe. William Lukuvi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na watendaji wa wizara hiyo walipomkaribisha rasmi yeye na Naibu Waziri wake katika ofisi za wizara hiyo.
Mhe. Lukuvi amewataka watendaji wa wizara yake kufanya kazi ya kuhakiki ripoti za hati na umiliki wa ardhi kwa wiki moja na jumatatu ijayo wanatakiwa kutoa majibu ya maswali yote atakayoyauliza katika idara mbalimbali za kiutendaji katika wizara hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa hawatakuwa tayari kuona mwananchi yeyote akinyanyaswa kuhusiana na matumizi kandamizi ya ardhi.