Tuesday , 13th Jan , 2015

Wananchi wenye ulemavu wa kuzungumza na kusikia wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wanashindwa kupata huduma za kijamii kutokana na maeneo hayo kutokuwepo na watoa huduma wenye taaluma ya lugha ya alama.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw, Nyirembe Munasa.

Wakizungumza kupitia kwa mkalimani wao wananchi hao wakiwemo vijana waliopata elimu katika vyuo mbalimbali wamesema tatizo hilo pia linasababisha washindwe kupata ajira katika ofisi za serikali na watu binafsi kutokana na kushindwa kuelewana na wanaohusika.

Akizungumzia tatizo hilo mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa amesema serikali wilayani humo imeshaanza kushughulikia tatizo hilo na imeshapata mwekezaji wa kusaidia kuboresha chuo cha elimu maalumu cha patandi ili kisaidie kupata walimu wa kusaidia tatizo hilo.

Baadhi ya wananachi wamesema kutokana na ugumu wa maisha walemavu wengi hasa wa vijijini wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mahitaji muhimu kama vile baiskel za fimbo na mafuta kwa walemavu wa ngozi.